Ua lililopandwa katika kona ya nyumba upande wa nje nakunawiri |
nakshi ya mazingira ya nyumbani
Itazungumzia jinsi maua na bustani yanavyoweza kuongeza uzuri wa mazingira ya nyumba.
Friday, 24 April 2015
Thursday, 23 April 2015
Habari za wakati huu mfuatiliaji wa blog hii, ni wakati muafaka wa kwenda kujua maua yanayofaa katika kupanda kwenye kiunga arthini na kutambaa kuifunika ardhi isionekane, aina hii huota chini kwa kutambaa pia maua ya aina hii yapo ya aina tofauti kuna yale yanayo toa maua ya rangi na yale yanayoota na kutoa rangi moja tu, kama ni la rangi yakijani basi halibadiliki na kama linatoa maua ya rangi mchanganyiko litaendelea na asili yake.
Pia unaweza ukapanda maua ya kutambaa na baadhi ya maeneo ukapanda maua ya miti hii huongeza naksi ya mazingira ya nyumba yako, kwa kutazama picha utaona namna ya kufanikisha zoezi hili, na kuvutiwa pia kuchukua hatua katika mjengo wako.
huo ni mfano wa mauwa ya kutambaa yaliyochanganywa na maua ya miti. |
yafuatayo ni mauwa ya kutambaa yalipandwa peke yake katika kiunga na kuboresha muonekano
maua yanayoota kwa kutoa aina tofauti za rangi na yanaota kwa kutambaa ardhini |
Wednesday, 22 April 2015
Habari mpya wapendwa wafuatiliaji wa blog hii, je wajua waweza pamba muonekano wa mlango wako kwa maua?
leo tutaona jinsi maua yanavoweza kuweka muonekano mzuri wa mlango wako hasa mlango wakioo ukitazama kwa makini picha hiyo hapo chini ni namna gani hili ua lililopandwa kwenye kopo jinsi linavyo vutia, nakuifanya nyumba kuwa na nakshi nzuri.
kwa aina tofauti na za kuvutia usichoke kufuatilia usipitwe na wakati, nakshi ya mazingira nyumbani hufurahisha wageni toka wanapo ingia ndani kwako ta kutoka pia kwasababu aina tofauti za maua yako huwafanya watu kuitazama mara kwa mara.
Friday, 17 April 2015
muonekano wa ua lililopandwa kwenye kopo na lililopandwa ardhini lakini yote kuwa katika hali moja kutokana na usimamizi mzuri,ua lilipandwa kwenye kopo huweza kuhamishwa na kuliweka ndani ya nyumba kwa mda kadhaa na kulitoa ililiweze kupata hewa ya asili.
huo ni muonekano wa maua yaliyo pandwa katika ardhini na yaliyopandwa katika makopo,
Thursday, 16 April 2015
Katika
kuangazia upambaji wa nyumba yako kwa maua ya asili leo tutaangalia jinsi mti
mmoja wa maua wenye aina tofauti za rangi katika matawi yake na unavyoweza kuweka mazingira yako
yakawa ya tofauti kwa mchanganyiko wa rangi zake.
Maua
hayo kwa muonekano wake unaweza ukaona kama yamechanganywa kumbe sivyo, bali ni
asili yake katika uotaji wake.
ua la kwanza kwa muonekano wake lina rangi tatu kijani, njano na zambarau hizo rangi hazijatengenezwa bali ni asili yake.
maua yanayoonekana namba mbili pia yana aina tofauti za rangi kama yanavyoonekana hapo juu. ua linaloonekana katika kihifadhio chake wanawake wengi hupenda kuliita ua kitenge kutokana na mchanganyiko wa rangi zake kama kilivyokuwa kitenge.
Wednesday, 15 April 2015
maua ya asili katika upambaji wa mazingira ya nyumbani
Maua
ni mapambo ambayo watu wengi hupenda kuyatumia katika urembo na mapambo kwa
mazingira tofautitofauti, kwa mtazomo chanya watu hupenda kusema kua maua
huweza kuongeza uzuri wa eneo na kuliweka katika hali ya kupendeza Zaidi kwa rangi tofautitofauti
zilizochanganywa.
Kwa upande wa blog hii tutakwenda moja kwamoja
kufahamu zaidi kuhusiana na maua ya asili katika hupendezesha nyumba hasa yakiwa katika
mpangilio mzuri katika viunga au makopo yalimo hifadhiwa na kutuzwa kwa umakini
na kujua namna ya kuyatunza, ili maua yawezae kunawili na kupendeza ni lazima
ya pewe kipaumbele katika kuyatuza kama kiumbe hai kwakuwa hayana uwezo wa
kujitunza katika swala zima la kujitafutia chakula, kawaida ya maua ya porini
hunawiri wakati wa masika na kusinyaa wakati wa kiangazi, hivyo basi katika
kuhakikisha maua ya kupandwa yanakuwa yenye afya wakati wote cha muhimu ni
kuyamwaguia maji na kuyalisha chakula kama kiumbe hai chakula cha maua ya
bustani si kama tunavyofikiria kuwa chakula huandaliwa jikoni na kuandaliwa
kwaajili ya ulaji bali maua yanahidaji samadi mbalimbali ikiwamo vinyesi vya wanyama
kama ng”ombe mbuzi nawengineo, ili kurutubisha mimea iwe yenye uwezo wa
kuhimili haliyoyote ile ya hewa.
Je?utawezeshaje maua yako kunawili wakati wote.
·
Ili
maua yaweze kunawiri wakati wote yamwagiliwe maji mara mbili kwa siku asubuhi na
jioni.
·
Yasafishwe
mara kwa mara kwa kutoa matawi yaliyo nyauka na kuyaacha yenye afya tu.
·
Kamanimaua
yaliyopandwa kwenye makopo kopo liache matundu madogomadogo chini na pembeni
ili yaweze kuchuja maji yasioze.
·
Na
kwayale yaliyopandwa kwenye viunga ardhini yatifuliwe kila baada ya muda ili
maji yapite vizuri kuifikia mizizi.
·
Ua
litakapo kaa kwa muda mrefu litolewe na kubadilisha lianze upya.
yafuatayo ni maua yaliyo pandwa kimpangilio kutokana na eneo husika na kutunzwa vyema.
Subscribe to:
Posts (Atom)