Wednesday, 15 April 2015

maua ya asili katika upambaji wa mazingira ya nyumbani



Maua ni mapambo ambayo watu wengi hupenda kuyatumia katika urembo na mapambo kwa mazingira tofautitofauti, kwa mtazomo chanya watu hupenda kusema kua maua huweza kuongeza uzuri wa eneo na kuliweka katika hali ya kupendeza Zaidi kwa rangi tofautitofauti zilizochanganywa.
 Kwa upande wa blog hii tutakwenda moja kwamoja kufahamu zaidi kuhusiana na maua ya asili katika  hupendezesha nyumba hasa yakiwa katika mpangilio mzuri katika viunga au makopo yalimo hifadhiwa na kutuzwa kwa umakini na kujua namna ya kuyatunza, ili maua yawezae kunawili na kupendeza ni lazima ya pewe kipaumbele katika kuyatuza kama kiumbe hai kwakuwa hayana uwezo wa kujitunza katika swala zima la kujitafutia chakula, kawaida ya maua ya porini hunawiri wakati wa masika na kusinyaa wakati wa kiangazi, hivyo basi katika kuhakikisha maua ya kupandwa yanakuwa yenye afya wakati wote cha muhimu ni kuyamwaguia maji na kuyalisha chakula kama kiumbe hai chakula cha maua ya bustani si kama tunavyofikiria kuwa chakula huandaliwa jikoni na kuandaliwa kwaajili ya ulaji bali maua yanahidaji samadi mbalimbali ikiwamo vinyesi vya wanyama kama ng”ombe mbuzi nawengineo, ili kurutubisha mimea iwe yenye uwezo wa kuhimili haliyoyote ile ya hewa.

Je?utawezeshaje maua yako kunawili wakati wote.

·         Ili maua yaweze kunawiri wakati wote yamwagiliwe maji mara mbili kwa siku asubuhi na jioni.
·         Yasafishwe mara kwa mara kwa kutoa matawi yaliyo nyauka na kuyaacha yenye afya tu.
·         Kamanimaua yaliyopandwa kwenye makopo kopo liache matundu madogomadogo chini na pembeni ili yaweze kuchuja maji yasioze.
·         Na kwayale yaliyopandwa kwenye viunga ardhini yatifuliwe kila baada ya muda ili maji yapite vizuri kuifikia mizizi.
·         Ua litakapo kaa kwa muda mrefu litolewe na kubadilisha lianze upya.
yafuatayo ni maua yaliyo pandwa kimpangilio kutokana na eneo husika na kutunzwa vyema.



No comments:

Post a Comment