Thursday, 16 April 2015

Katika kuangazia upambaji wa nyumba yako kwa maua ya asili leo tutaangalia jinsi mti mmoja wa maua wenye aina tofauti za rangi katika matawi yake na unavyoweza kuweka mazingira yako yakawa ya tofauti kwa mchanganyiko wa rangi zake.


Maua hayo kwa muonekano wake unaweza ukaona kama yamechanganywa kumbe sivyo, bali ni asili yake katika uotaji wake.
ua la kwanza kwa muonekano wake lina rangi tatu kijani, njano na zambarau hizo rangi hazijatengenezwa bali ni asili yake.
maua yanayoonekana namba mbili  pia yana aina tofauti za rangi kama yanavyoonekana hapo juu. ua linaloonekana katika kihifadhio chake wanawake wengi hupenda kuliita ua kitenge kutokana na mchanganyiko wa rangi zake kama kilivyokuwa kitenge.

No comments:

Post a Comment