Friday, 24 April 2015

Ua lililopandwa katika kona ya nyumba upande wa nje nakunawiri


Thursday, 23 April 2015

Habari za wakati huu mfuatiliaji wa blog hii, ni wakati muafaka wa kwenda kujua maua yanayofaa katika kupanda kwenye kiunga arthini na kutambaa  kuifunika ardhi isionekane, aina hii huota chini kwa kutambaa pia maua ya aina hii yapo ya aina tofauti kuna yale yanayo toa maua ya rangi na yale yanayoota na kutoa rangi moja tu, kama ni la rangi yakijani basi halibadiliki  na kama linatoa maua ya rangi mchanganyiko litaendelea na asili yake.
Pia unaweza ukapanda maua ya kutambaa na baadhi ya maeneo ukapanda maua ya miti hii huongeza naksi ya mazingira ya nyumba yako, kwa kutazama picha utaona namna ya kufanikisha zoezi hili, na kuvutiwa pia kuchukua hatua katika mjengo wako.

huo ni mfano wa mauwa ya kutambaa yaliyochanganywa na maua ya miti.



yafuatayo ni mauwa ya kutambaa yalipandwa peke yake katika kiunga na kuboresha muonekano

maua yanayoota kwa kutoa aina tofauti za rangi na yanaota kwa kutambaa ardhini

 

Wednesday, 22 April 2015

Habari mpya wapendwa wafuatiliaji wa blog hii, je wajua waweza pamba muonekano wa mlango wako kwa maua?
leo tutaona jinsi maua yanavoweza kuweka muonekano mzuri wa mlango  wako hasa mlango wakioo ukitazama kwa makini picha hiyo hapo chini ni namna gani hili ua lililopandwa kwenye kopo jinsi linavyo vutia, nakuifanya nyumba kuwa na nakshi nzuri.

kwa aina tofauti na za kuvutia usichoke kufuatilia usipitwe na wakati, nakshi ya mazingira nyumbani hufurahisha wageni toka wanapo ingia ndani kwako ta kutoka pia kwasababu aina tofauti za maua yako huwafanya watu kuitazama mara kwa mara.

Friday, 17 April 2015

muonekano wa ua lililopandwa kwenye kopo na lililopandwa ardhini lakini yote kuwa katika hali moja kutokana na usimamizi mzuri,ua lilipandwa kwenye kopo huweza kuhamishwa na kuliweka ndani ya nyumba kwa mda kadhaa na kulitoa ililiweze kupata hewa ya asili.

huo ni muonekano wa maua yaliyo pandwa katika ardhini na yaliyopandwa katika makopo,

Thursday, 16 April 2015

Katika kuangazia upambaji wa nyumba yako kwa maua ya asili leo tutaangalia jinsi mti mmoja wa maua wenye aina tofauti za rangi katika matawi yake na unavyoweza kuweka mazingira yako yakawa ya tofauti kwa mchanganyiko wa rangi zake.


Maua hayo kwa muonekano wake unaweza ukaona kama yamechanganywa kumbe sivyo, bali ni asili yake katika uotaji wake.
ua la kwanza kwa muonekano wake lina rangi tatu kijani, njano na zambarau hizo rangi hazijatengenezwa bali ni asili yake.
maua yanayoonekana namba mbili  pia yana aina tofauti za rangi kama yanavyoonekana hapo juu. ua linaloonekana katika kihifadhio chake wanawake wengi hupenda kuliita ua kitenge kutokana na mchanganyiko wa rangi zake kama kilivyokuwa kitenge.

Wednesday, 15 April 2015

maua ya asili katika upambaji wa mazingira ya nyumbani



Maua ni mapambo ambayo watu wengi hupenda kuyatumia katika urembo na mapambo kwa mazingira tofautitofauti, kwa mtazomo chanya watu hupenda kusema kua maua huweza kuongeza uzuri wa eneo na kuliweka katika hali ya kupendeza Zaidi kwa rangi tofautitofauti zilizochanganywa.
 Kwa upande wa blog hii tutakwenda moja kwamoja kufahamu zaidi kuhusiana na maua ya asili katika  hupendezesha nyumba hasa yakiwa katika mpangilio mzuri katika viunga au makopo yalimo hifadhiwa na kutuzwa kwa umakini na kujua namna ya kuyatunza, ili maua yawezae kunawili na kupendeza ni lazima ya pewe kipaumbele katika kuyatuza kama kiumbe hai kwakuwa hayana uwezo wa kujitunza katika swala zima la kujitafutia chakula, kawaida ya maua ya porini hunawiri wakati wa masika na kusinyaa wakati wa kiangazi, hivyo basi katika kuhakikisha maua ya kupandwa yanakuwa yenye afya wakati wote cha muhimu ni kuyamwaguia maji na kuyalisha chakula kama kiumbe hai chakula cha maua ya bustani si kama tunavyofikiria kuwa chakula huandaliwa jikoni na kuandaliwa kwaajili ya ulaji bali maua yanahidaji samadi mbalimbali ikiwamo vinyesi vya wanyama kama ng”ombe mbuzi nawengineo, ili kurutubisha mimea iwe yenye uwezo wa kuhimili haliyoyote ile ya hewa.

Je?utawezeshaje maua yako kunawili wakati wote.

·         Ili maua yaweze kunawiri wakati wote yamwagiliwe maji mara mbili kwa siku asubuhi na jioni.
·         Yasafishwe mara kwa mara kwa kutoa matawi yaliyo nyauka na kuyaacha yenye afya tu.
·         Kamanimaua yaliyopandwa kwenye makopo kopo liache matundu madogomadogo chini na pembeni ili yaweze kuchuja maji yasioze.
·         Na kwayale yaliyopandwa kwenye viunga ardhini yatifuliwe kila baada ya muda ili maji yapite vizuri kuifikia mizizi.
·         Ua litakapo kaa kwa muda mrefu litolewe na kubadilisha lianze upya.
yafuatayo ni maua yaliyo pandwa kimpangilio kutokana na eneo husika na kutunzwa vyema.